Thursday, 21 April 2016

Mabasi yaendayo kasi yaanza safari zake Dar


Mabasi yaendayo kasi, yameanza kufanya safari zake katikati ya jiji la Dar es Salaam Ijumaa hii.
31
Jumla ya mabasi 50 yameingia barabarani. Kwa wewe ambaye hujui njia mbalimbali za mabasi hayo, chini ni sehemu yanapopita.
1) RUTI YA KIMARA- KIVUKONI Mabasi Sita (6). Kati ya mabasi Hayo sita wakati wa Kutoka Jangwani matatu yataenda Kimara na Matatu Kivukoni.
2. RUTI YA KIMARA – KARIAKOO Mabasi Sita (6). Kati ya hayo Matatu yataelekea Kariakoo na Matatu Kimara.
3. RUTI YA UBUNGO – KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi Manne yataelekea Ubungo na Manne Kivukoni.
4. RUTI YA UBUNGO – KARIAKOO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi manne Yataenda Ubungo na Manne yataenda Kariakoo.
5. RUTI YA UBUNGO – MOROCCO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Manne yataenda Ubungo Manne yataenda Morocco.
6. RUTI YA MOROCCO – KARIAKOO Mabasi sita (6). Kati ya hayo mabasi Matatu Morocco na Matatu Kariakoo.
7. RUTI YA MOROCCO – KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya Hayo Mabasi Manne yataenda Moroco na mabasi manne Kivukoni.
DESPATCH PLAN SAA KUMI NA MBILI KAMILI. 1. Kimara Terminal Mabasi Sita (6) 2. Ubungo Terminal Mabasi kumi na mbili (12) 3. Morocco Termial Mabasi kumi na moja (11) 4. Kariakoo Terminal Mabasi kumi (10) 5. Kivukoni Terminal Mabasi kumi na moja (11) JUMLA NI MABASI HAMSINI (50)
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: