Wednesday, 20 April 2016

Siku 27 za rapper Chid Benz ndani ya Sober House Bagamoyo




Headlines za msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Ilala, Rashid Makwilo aka Chid Benz  zilichukua ukurasa kwenye mitandao mbalimbali za kujihusisha na madawa ya kulevya.
Sasa kama unakumbuka March 22, 2016 meneja wa Diamond Platnumz alimpeleka rapper huyo Sober House iliyopo Bagamoyo iitwayo Life and Hope Rehabilitation Centre kwaajili ya kupata matibabu ya kuacha kutumia madawa hayo na kurudi kwenye hali yake ya mwanzo.
KALAPINA
Kupitia kwenye ukurasa wa msanii wa Hip Hop Kalapina ambaye anaendesha kipindi cha harakati cha kupinga utumiaji wa Madawa ya kulevya alipost video yenye sekunde 15 zikimuonesha Chid Benz baada ya kukaa Sober House  siku 27 na kuandika..’Ni safari ya chid benz na harakati na hapa ni siku 27 ndani ya sober house mshkaji anaendelea vizuri sana kilichobaki ni kumuombea kwa mungu asiweze kurejea tena katika matumizi ya dawa za kulevya safari nzima ya chid benz utaiona kupitia kipindi cha harakati cloudstv stay tune’- Kalapina
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: