Tuesday, 3 May 2016

Ungependa kujua nyota yako au ya rafiki yao na tabia zake? Soma hapa


Mimi sio mtabiri wa nyota wala sina elimu yoyote ya nyota, lakini kitu kimoja nimejifunza ni kusoma tabia za watu kwa kutumia nyota zao,nyota zimepangwa katika mafungu 12 na kila nyota ina sifa ambazo zingine zinafanana na mtu wenye nyota hiyo japokuwa si mara zote, ukijua sifa hizi itakuwa raisi kumtambua mtu wako wa karibu na tabia zake nilitafuta sifa hizi kurahisisha kazi tuangalie kila nyota na sifa zake,
Kondoo/Punda (Aries) Mach 21 – Apr 19
Kondoo ndio nyota ya kwanza katika nyota zote na wanapenda kuwa wa kwanza katika kila kitu, wacheshi sana ila wana hasira za karibu sana, wanakuaga na vipaji na wabunifu  hawapendi kushindwa,hawapendi kusubiri kwa chochote, Kwa ujumla wenye nyota ya Punda ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kubwa hawapendi kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. Ni watu wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali kushindwa.
Ng’ombe (Taurus )  Apr20 – Mei 20
Kama ilivyo kwa ngo’ombe watu wa nyota hii ni watulivu ila wakorofi wakichokozwa,wanapenda maisha mazuri,fedha magari na nyumba nzuri, wanajituma sana kazini sio watu wanaoingia katika mahusiano kiraisi ila wakiingia wanakuwa waaminifu sana, pia ni viongozi wazuri. Pamoja na hisia kali walizonazo, wao ni watu imara na wasiobadilika hivyo kuwafanya watu wenye shauku kutovutiwa nao.
Uaminifu ni jambo la pili ambalo wenye nyota hii wanalo hivyo kuwafanya wao wawe watu wenye kuaminika na hiyo inasababisha wawe wenye wivu kupindukia.
Mapacha (Gemini) Mei 21 – Jun 20
Hawa ni watu wa watu wanapenda kujichanganya, na kuwa na watu mda wote kama nyota ilivyo mapacha mtu mwenye nyota hi hapendi awe pekeake pekeake, wanapenda kushea mawazo na watu kukutana na marafiki wapya na kusafiri wanapenda sana kuonekana kwenye mapenzi huwa hawapendi watu wanaowaboa, hawa huwa wanachukia mahusiano yanayoboa Ni watu wenye asili ya mawasiliano na ni vigumu sana kuwafanya wajinga hivyo basi wakishampenda mtu wanahakikisha kwamba hawamchoshi huyo mpenzi. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.
Kaa (Cancer ) Jun 21- Jul 22
Watu wa nyota hii wanapenda sana familia zao,wanapenda kuwa karibu na vitu vinavyowapa raha na kuwafurahisha,wana aibu kidogo ila wanapenda kuwa watu ambao watahitajika na wengine sababu wanajali sana,wasikivu, ni marafiki wazuri kuwa nao karibu
Wenye Nyota hii bila ya kuwa na mpenzi hujihisi hawajatimiza lengo lao katika maisha hivyo basi huwa hawana raha.Ni wapenzi waaminifu na wanategemea wapenzi nao wawe waaminifu kama wao.Ni wagumu sana kuachana na wapenzi na inapotokea huwa hawaagi wako radhi wao waumie kuliko kuachana na anayempenda.

Simba (Leo) Jul 23 – Ag 22
Kama alivyo simba wanapenda kuwa viongozi na wanapenda kusikilizwa,wanapenda kuonekana wanaongoza kila sehemu,waaminifu wana mapenzi ya kweli na hawapendi dharau,wanapenda maisha ya kifahari sana, wana mvuto kwa wengine wana uwezo wa kukaa kwenye mahusiano mda mrefu. Wanapenda kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika basi inakua vigumu sana kuyatengeneza.
Tatizo lao kubwa ni wao kujisahau kwamba ni upande mmoja wa penzi na wanajifanya wao ndio viongozi.
Mashuke (Virgo) Ag 23 – Sept 22
Watu wakufikiria sana watulivu wanapenda kufanya mambo yao chini kwa chini,wanapenda kuwa peke yao,wanapenda kufanya kazi kwa mikono yao ni wabunifu,wanapenda sana familia na watoto. Ni watu ambao inawawia vigumu kuonyesha penzi lao. wana mtizamo wa kufikiri kabla ya kujitumbukiza ndani ya penzi lolote, wanachunguza kwa makini matokeo ya penzi lenyewe,ila wanapenda sana kulalamika na kukosoa wengine
Mizani  (Libra) Sept 23- Okt 22
Hawa wanapenda sana kuweka kila kitu sawa kama ilivyo mzani hawapendi uonevu na ni watu washeshi wanapenda sana amani wanapenda kumfanya mtu ajisikie vizuri kama yupo kwenye matatizo na watu hawaboi kuwa katikati ya watu.wapo tayari kufanya kila kitu kwa ajiri ya kumfanya mtu awe na furaha hasa katika familia zao. Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
N’ge  (scorpio) Okt 23 – Nov 21
Watunza siri wanapenda kuweka vitu moyoni sana,wanapenda uongozi,wanaweza kusimama kwa wale wasioweza kujisimamia na wanajaliNi watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja. Kwao mapenzi au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa kwamba nyota ya Nge inatawala sehemu za siri. Inashauriwa wale wenye moyo mdogo wasifanye mapenzi na Nge sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.
Mshale (Sagittarius) Nov 22 – Dis 21
Wanapenda sana kusafiri,wanajali sana marafiki na watu wao wa karibu,wana marafiki wengi,wanapenda kuuliza sana maswali kuhusu kila kitu. Ni watu wanaopenda kufanya ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali na inashauriwa kwamba wapenzi wao wawe wamekula kabla ya tendo la ndoa vinginevyo itakuwa taabu.wanapenda sana uhuruWanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni wanakuwa wagumu sana kujihusisha. Wanapenda sana wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.
Mbuzi  (Capricorn) Dis 22-  Jan 19
Wako makini sana kimaisha,wanafanya sana kazi kwa makini,wanatafuta mafanikio kwa nguvu wako vizuri sana kwenye hesabu, wanapenda kuwa katika familia zilizo na mshikamano hawapendi ugomvi na manyanyaso  Ni watu wanaoogopa sana kuachwa na wapenzi wao hivyo basi huwa wanakuwa waangalifu sana katika kuchagua wapenzi. Jambo jingine ni kuwa huwa wao wenyewe hawajiamini kimapenzi, mara nyingi wanashindwa kuingia katika mapenzi kwa woga tu hivyo kukosa nafasi nzuri ya kupendwa.

Ndoo (Aquarious) Jan 20 – Feb 18
Wana uwezo wa kuwa na marafiki wengi,ila wanapenda pia kujitenga wakati mwingine sio watu wenye hisia sana, wanapenda sana kushea mawazo yao na wengineWako tayari kutulia katika mapenzi iwapo watahakikishiwa uhuru wao na haki ya kutoingiliwa katika mambo binafsi. Niwa watu ambao hawapendi kuonyesha hisia zao halisi na wanachukua muda mrefu kuingia kikamilifu katika uhusiano wa kimapenzi.

Samaki (Pisces) Feb 19 – Mach 20
Wana huruma sana,wanajali sana hawapendi kuumiza wengine na wanapenda kuhakikisha wengine wako na furaha wanafisha sana hisia zao, wanajituma sana,wanapenda kufikiria vitu vikubwa na mawazo makubwa ya kimaendeleoTatizo lao kubwa la kimapenzi ni kwamba wanawaamini sana wapenzi wao na wanakuwa na mawazo au firika za kimapenzi ambazo hazipo katika dunia hii. Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokuwa katika mapenzi wanakuwa wamejawa na shauku na mifano ya kuvutia na wanapenda wapenzi wao waishi kiroho. Mategemeo yao yanakuwa makubwa na yasipotimia huwa wanavunjika moyo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: