Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) ya kufutiwa mashitaka ya
uchochezi yanayomkabili na wenzake watatu.
Tundu Lissu na wenzake kupitia kwa
wanasheria wao waliwasilisha maombi yao katika mahakama hiyo ya kutaka
mahakama kufuta mashtaka hayo kwa madai kuwa hati ya mashtaka imekosewa
kwani haielezi vya kutosha kuhusu makosa wanayotuhumiwa kuyatenda.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilieza
jana kuwa baada ya kupitia hoja za pande zote mbili (mshataki ambaye ni
Jamhuri na mshtakiwa ambaye ni Tundu Lissu na wenzake) walijiridhisha
kuwa hati hiyo haina makosa.
Watuhumiwa wanakabiliwa na mashtaka ya
kuchapisha habari ya uchochezi kwenye gazeti yenye kichwa cha habari
kilichosomeka “Machafuko Zanzibar”. Habari hii ilichapishwa kati ya
Januari 12-14 mwaka huuna inadaiwa ililenga kuwatisha wananchi wa
Zanzibar wasijitokeze kwenye uchaguzi wa marudio Machi 20 mwaka huu.
Pamoja na na Tundu Lissu, washtakiwa
wengine ni pamoja na mwandishi wa gazeti la Mawio, Jabir Idrissa,
Mhariri wa gazeti hilo, Simon Mkina na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana,
Ismail Mehboob.
0 comments: