Leo August 23 2016 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi amekutana na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa
katika awamu ya pili madawati 20,000 yameshakamilika na yanaweza
kuchukuliwa kuanzia sasa kwenda kwenye majimbo yaliyopangiwa kupata
madawati hayo.
Katika
kutekeleza mpango huo, awamu ya kwanza jumla ya madawati 32,387
yalitengenezwa na yaliyochukuliwa na Wabunge kwa kushirikiana na
Halmashauri zao ni 22,721 tu, hivyo madawati 9,666 sawa na asilimia 30%
bado hayajachukuliwa na Majimbo husika.
Akizungumzia
Majimbo ambayo hayajachukua madawati yake katika awamu ya kwanza Dkt.
Mwinyi amesema ni vyema Viongozi katika Majimbo hayo wakiwemo wabunge
wanatakiwa wakachukue madawati hayo ndani ya siku 7 ambapo mwisho
itakuwa August 30 2016
Majimbo
ambayo hayajachukua madawati yake katika awamu ya kwanza yametajwa kuwa
ni Kilindi, Pangani, Makambako, Ludewa, Wangingombe na Makete. Majimbo
mengine ni Kyela, Rungwe, Busokelo, Songwe, Kwela, Tunduru, Iringa
Mjini, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini na Ileje Nkasi Kaskazini na Nkasi
Kusini.
0 comments: