Monday, 28 April 2014

KIJANA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUDANDIA TAIRI YA NDEGE NA KUSAFIRI MASAA 5

Kijana huyo aliyenusurika kifo wakati wa safari yake ya saa tano angani , amepigwa na mshangao kujua kuwa kijana wake yuko hai na kuwa alipanda ndege hiyo akidhani ilikuwa inaeleklea Somalia, ili aweze kurejea nyumbani.

Mama huyo, Ubah Mohamed Abdullahi, anayeishi katika kambi ya wakimbizi nchini Ethiopia, anasema kuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kusikia kuhusu kijana wake ambaye alipotea miaka sita iliyopita.
Mama Uba ambaye alitalakiana na mumewe, alisema hakuwahi kuwasiliana na familia yake yake iliyohamia nchini Marekani mwaka 2008.
Babake kijana huyo menye umri wa miaka 16 alisema kuwa alikuwa anajaribu kurejea Somalia na kwamba alidhani ndege hiyo ilikuwa inaelekea Somalia ili aweze kwenda kumuona mamake.
Yahya Abdi alisafiri bila ya hewa ya Oksijeni akiwa angani kwenye baridi kali kwa saa tano kutoka Carlifonia hadi Hawaii


Mama Abdullahi alisema kuwa alipokea taarifa kutoka kwa jamaa wake wanaoishi Ulaya kuhusu mtoto wake na alivyonusurika kifo.
Akiongea na BBC kutoka katika kambi ya wakimbizi ya Sheed Dheer ambako amekuwa akiishi tangu mwaka 2008,mama huyo Abdullahi alisema kuwa alishangazwa sana na mwanawe ambaye alihatarisha maisha yake kwenda kumtafuta.
Alisema kuwa tangu wanawe na baba yao kwenda Marekani,, amekuwa akijaribu sana kuwatafuta bila mafanikio.
Baada ya Yahya Abdi kupatikana akiwa katika uwanja wa kutua ndege aliambia mafisa wa usalama kuwa alikuwa ametofautiana na famia yake nyumbani na ndio maana akaamua kuchukua ndege ya kwanza aliyopitaka kurejea Somalia.
Katika mahojiano na shirika la habari la Voice of America, babake kijana huyo Abdilahi Yusuf Abdi, alisema kuwa Mungu alimuokoa mwanawe ambaye daima alikuwa anataka kurejeaAfrika
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: