MFANYABIASHARA
maarufu wa simu za mikononi maeneo ya Kariakoo jijini Dar,
aliyefahamika kwa jina moja la Devi, hivi karibuni alipatwa na soni ya
aina yake baada ya kukutwa katika nyumba ya kulala wageni akiwa na mke
wa rafiki yake wa karibu.
Licha ya kukuta ujumbe huo wa kimahaba, chanzo chetu kilidai kuwa pia mume huyo alikutana na sms kadhaa zilizokuwa zimetuma fedha kwa njia ya mtandao wa simu, zikielekezwa kwa dada huyo kwa ajili ya matumizi yake.
Baada ya jamaa huyo kujiridhisha kuwa Davi alikuwa na nia mbaya na mkewe, mume huyo aliamua kuanzisha mkakati na kumtuma mdogo wake kufuatilia ishu nzima kwani yeye alibanwa na majukumu mengine ya kikazi.
Bila kujua kuwa nyendo zao zinafuatiliwa, Davi na shemeji yake walipanga kukutana katika hoteli moja (jina linahifadhiwa)iliyopo Sinza na baada ya kupata chumba na kuingia ndani, bila hofu, walianza kujiandaa kwa ajili usaliti.
Huku mwanaume akiwa ameshatoa nguo zake sambamba na mpenzi wake, mlango wa chumba chao uligongwa, lakini wakiwa hawana hofu,wakiamini ni mhudumu walifungua na wote kupatwa na bumbuazi baada ya kugundua aliyekuwa mbele yao ni mdogo wa mwenye mke ambaye wote wanamfahamu!
“Huwezi kuamini, baada ya sisi kuingia chumbani na kuwakuta kama walivyozaliwa, jamaa alikimbilia chooni na kwa jinsi alivyokuwa, alionyesha kabisa kuhitaji kujitumbukiza, lakini bahati nzuri vyoo vile ni vya kisasa,” kilidai chanzo hicho.
Mwandishi wetu alimtafuta kwa njia ya simu mwenye mke kutaka kujua kilichoendelea baada ya tukio hilo ambapo alipopatikana alisema:
“Ni kweli tukio hilo limetokea ila siwezi kuzungumzia zaidi, jamaa alikuwa akinizunguka kwa mke wangu lakini arobaini yake imefika, zaidi nenda Kituo cha Polisi Oysterbay utaelezwa kila kitu.”
Mfanyabiashara
maarufu wa simu za mikononi maeneo ya Kariakoo jijini Dar,
anayefahamika kwa jina moja la Devi baada ya kufumaniwa na mke wa
rafikiye.
Mtoa habari makini aliliambia gazeti hili kuwa kisa kizima kilianza
baada ya mwenye mali (mume) kukuta ujumbe mfupi wa simu katika
kilongalonga cha mkewe unaoashiria mambo ya mapenzi na mbaya zaidi,
meseji hiyo ilitoka kwa rafiki yake huyo.Licha ya kukuta ujumbe huo wa kimahaba, chanzo chetu kilidai kuwa pia mume huyo alikutana na sms kadhaa zilizokuwa zimetuma fedha kwa njia ya mtandao wa simu, zikielekezwa kwa dada huyo kwa ajili ya matumizi yake.

0 comments: