Msichana huyo aliishi na Tumbili kwenye chumba cha kueegesha magari
Polisi nchini Argentina
wamemwokoa msichana mwenye umri wa miaka kumi na mitano ambaye
alifungiwa katika chumba cha kuegesha magari na kunyimwa chakula pamoja
na kupigwa na wazazi waliokuwa wamemuasili, kwa kipindi cha miaka tisa.
Msichana huyo alikuwa na uzani wa kilo ishirini pekee.Amesema alifanikiwa kuondoka katika eneo hilo la kuegesha magari mara mbili tu katika kipindi cha miaka tisa.
Walezi wake wamekamatwa na kufunguliwa mashItaka ya kumdhulumu na kumweka kama mtumwa msichana huyo.
Msichana huyo ambaye amelazwa hospitlaini, alipatikana na dadake wa kuzaliwa naye mjini Buenos Aires.
Kwa mujibu wa maafisa wakuu, wazazi hao walimuasili mwaka 2001 baada ya mahakama kuamua kuwa wazazi wake wa kumzaa hawakuwa na uwezo wa kifedha kuweza kumlea.
Walikuwa wanasubiri stakabadhi za kukamilisha mpango wa kumuasili mtoto huyo.
0 comments: