Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika
kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na
dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa
Taifa letu.
Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi
binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na
Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979,
nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri
mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea
kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata
aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika
inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha
Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972.
Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana
na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992
na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema,
nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa
azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi
wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa
letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.
Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa
M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na
uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa
wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini
na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka
katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma
(Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna
Kulala Mpaka Kieleweke:
Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya
Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia
dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha
kwa unyofu wao.
Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!
With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD
TASTE.
Edwin Mtei,
Founder Chairman of CHADEMA.
0 comments: