Thursday, 17 April 2014

SHILOLE: NILIPONASA SASA SIPINDUI-MAHABA NINYONGE



Na Denis Mtima
STAA wa filamu na mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’ amefunguka kuwa amenasa vilivyo katika penzi la msanii mwenzake, Nuhu Mziwanda hatarajii kuachika.

Akipiga stori na paparazi wetu, Shishi alisema yupo tayari kuolewa na Mziwanda kwani anampenda na ndiyo ubavu wake kutokana na vile ambavyo amekuwa akimwonesha mapenzi ya kweli tofauti na wapenzi wake wote waliopita.

“Huyu ndiye shemeji yenu, ndiye mume wangu mtarajiwa, ninampenda na yeye ananipenda kwa hiyo Mungu akijalia soon tutakamilisha taratibu za ndoa,’’ alisema Shishi Baby.
GPL
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: