Miezi
kadhaa iliyopita tulishuhudia kocha wa zamani wa Manchester United Sir
Alex Ferguson akizua mijadala mingi kwenye vyombo vya habari kutokana na
vitu alivyoandika kwenye kitabu chake.
Hivi sasa beki Rio Ferdinand
ambaye anakaribia kuondoka ndani ya klabu ya Man United nae anajiandaa
kutoa kitabu chake ambacho kinatajwa kitafunua yote ya nyuma ya pazia
kuhusu utawala wa David Moyes.
Ferdinand, 35, anatarajiwa kuandika yote
yanayohusiana na maisha yake ya soka kwenye kitabu ambacho kitapewa jina
la ‘#2sides: Rio Ferdinand – My Autobiography.’
Kitabu chake kinatarajiwa kueleza kiundani
msimu mbovu kuliko yote ndani ya klabu hiyo kufuatia kuondoka kwa kocha
Alex Ferguson na timu kukabidhiwa kwa David Moyes ambaye alitimuliwa
wiki kadhaa zilizopita – huku wachezaji wakubwa kama Ferdinand wakitajwa
kuwa na mkono kwenye kutia mchanga kibarua cha Moyes.
Kitabu hicho kinatarajiwa kutoka October 2 na kinachapishwa na kampuni ya Blink Publishing.
0 comments: