Hata hivyo Swahiliworldplanet imefanikiwa kugundua siri ya kinachomfanya star huyo kuwa na figure hiyo, habari za uhakika zisizo na shaka ni kuwa Irene Paul anatumia diet maalum ya products za Aloe Vera ambazo inadaiwa hazina madhara ingawa ni vizuri mhusika kumuona daktari kwanza kabla ya kuanza kutumia. "Irene ana umbo zuri kwasababu anatumia diet maalum ya bidhaa za Aloe vera, unajua Irene hapendi kunenepa hovyo ndiyo maana yupo kwenye shape kwa muda mrefu" kilisema chanzo kimoja cha kuaminika ambacho kipo karibu na star huyo wa filamu za Love Power, Handsome Wa Kijiji na Unpredictable.
Muigizaji kuwa na umbo la kawaida na kufanya mazoezi na diet mara kwa mara si tu kuwa humfanya apendeze kirahisi anapovaa nguo mbalimbali bali humfanya pia kuwa rahisi kucheza characters mbalimbali kwa urahisi katika filamu bila kusahau kuwa mazoezi na diet nzuri humlinda mtu na magonjwa hivyo kuwa fit kiafya muda wote.
Irene Paul |
0 comments: