kati mwinjilisti Reuben Kigame ambaye pia ni mkurugenzi wa Fish Fm radio kutoka pale Eldoret nchini Kenya. Reuben ana ulemavu wa macho (kipofu) lakini Mungu amemjaalia kipawa cha ajabu katika utunzi, uimbaji na upigaji. Kutoka kwa gwiji huyu tumekuchagulia wimbo 'Baba Yetu' ambao unapatikana katika album yake ya 'Ombi langu'.
Video imerekodiwa na kundi marafiki wa Kigame linaloitwa Sifa Voices la nchini Kenya ambao wamekuwa wakishirikishwa na Reuben kurekodi naye album mbalimbali. Reuben hajaonekana kwenye video hii, kutokana na kwamba huwa harekodi video kutokana na ulemavu wa macho alionao.
Natumaini utabarikiwa utazamapo na usikilizapo sauti na ujumbe huu unaopaza sifa kwa Mungu wetu, kwa matendo makuu na ya ajabu atutendeayo kila iitwapo leo. Barikiwa
0 comments: