Saturday, 10 May 2014

Exclusive: Rose Ndauka Kutolewa Mahari Na Malick Bandawe "Chiwa Man" Leo Hii.

Rose Ndauka na mchumba wake Malick Bandawe "Chiwa Man"
Hii ni exclusive! Star mkubwa wa filamu nchini anayetamba na filamu kibao sokoni Rose Ndauka anatolewa mahari leo hii baada ya kuwa katika uchumba na msanii mwenzake wa Bongofleva Malick Bandawe "Chiwa Man" kwa muda mrefu na kufanikiwa kupata mtoto wa kike miezi kadhaa iliyopita.
Chanzo kimoja cha kuaminika kilicho karibu na upande wa mume kimeitumia sms Swahiliworldplanet mchana huu kikisema "Rose Ndauka tunamtolea mahari leo". Chanzo hicho kilipododoswa tena kwa kuulizwa mahari ni kiasi gani na ndoa inategemewa kufanyika lini kilijibu kwa ufupi kwa kusema "We unanifanya niwe paparazi....sijui ni how much...nitakujibu later"

Rose Ndauka kutolewa kwa mahari inamaanisha kuwa harusi yake na Malick Bandawe ni hivi karibuni so watch this space for more.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: