SASA hakuna ubishi kuwa, ile ndoa
iliyofungwa kwa mbwembwe na kuvunjika kabla ya mwezi mmoja kati ya
msanii wa filamu za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ na Saad Omar, chanzo
ni Mwanabongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’.
Habari za awali zilisema kuwa, ndoa ya
Skaina iliingia mdudu baada ya mumewe kugundua kuwa alinunua ‘mbuzi
kwenye gunia’, kwani bidada huyo alikuwa na ujauzito wa mtu mwingine.
Hata hivyo, minong’ono ilikuwa inasema kuwa, mimba hiyo ilikuwa ya Nay ingawa awali, hakuna aliyekuwa tayari kufafanua kuhusiana na ishu hiyo.
Hata hivyo, minong’ono ilikuwa inasema kuwa, mimba hiyo ilikuwa ya Nay ingawa awali, hakuna aliyekuwa tayari kufafanua kuhusiana na ishu hiyo.
Ndoa ya wawili hao ilifungwa Oktoba 7,
2011 nyumbani kwa dada yake, Magomeni – Mapipa, Dar na kufika tamati
kabla ya mwezi Novemba, dah!
Ripoti zilizopo kwenye makabrasha ya
Risasi Mchanganyiko zinaonesha kuwa, baada ya Skaina kutemwa na Saad
alimweleza Nay sababu na kutimkia kwao Iringa ambapo alipojifungua
alimweleza ukweli mwenzi wake huyo kuhusu ujio wa mtoto wao.
Skaina.
Wawili hao wameelezwa kuwa na
mawasiliano ya karibu lakini ya siri kwa muda mrefu ila hivi karibuni,
wote waliamua kuutua mzigo huo na kuweka mambo hadharani ambapo kwa
upande wa Skaina alisema: “Nadhani mmechelewa tu kujua, lakini habari
ndiyo hiyo.”
Nay alipoulizwa, alijibu kwa kifupi sana: “Ni kweli lakini ni mambo ambayo huwa sipendi kuyazungumzia sana.”
Nay alipoulizwa, alijibu kwa kifupi sana: “Ni kweli lakini ni mambo ambayo huwa sipendi kuyazungumzia sana.”
Ili kuthibitisha ukweli huo, wikiendi
iliyopita, baada ya Nay kutwaa tuzo moja ya Kili katika kipengele cha
Wimbo Bora wa Kushirikiana, Skaina alitupia maneno ya kumpongeza Nay
katika ukurasa wake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram yaliyosema:
“Hongera baba mtoto wangu kwa kuchukua
tuzo, Mungu akuzidishie baraka na maisha marefu ili mwakani uweze
kuchukua tuzo nyingi zaidi. Navutiwa sana na kazi zako dady wetu
(akimaanisha yeye na mwanaye).”
Gpl
0 comments: