Ripoti
iliyotoka mwaka 2014 inayohusu idadi ya watu duniani ilionyesha China
ina watu bilioni 1.3..Katika vitu ambavyo walivifanya ili kupunguza watu
walipitisha sheria ya kila wanandoa mwisho wa kuzaa ni mtoto mmoja.
Kuna
hii nyingine imetokea nchini humo ambapo kampuni moja imepanga kutoa
masharti kwa wafanyikazi wake watakiwa kupata ruhusa kabla ya kupata
watoto.
Wanawake wote walio kwenye ndoa
wanaofikiria kupata watoto lazima wawe wamefanya kazi kwa mwaka mmoja
kwenye kampuni hiyo kabla ya kutuma kibali cha kukubaliwa kushika mimba.
Kama ikitokea umekiuka sheria hiyo atakayeshika mimba atatozwa faini na pia kushushwa cheo kama alikuwa nacho.
Shirika la utangazaji la China limekosoa vikali kampuni hiyo na kusema haina ubinadamu kwa wafanyikazi wake.
0 comments: