|
Uwoya |
Irene Uwoya ambaye ni mmoja wa mastaa wakubwa wa filamu nchini anadaiwa
kuwa katika penzi la siri kubwa na muigizaji mwenzake maarufu Haji Adam
"Baba Haji". Chanzo kimoja ambacho ni msanii chipukizi wa filamu
kilisema kuwa wawili hao ni wapenzi ila imekuwa vigumu hata media kujua
kwasababu mara nyingi hujifanya ukaribu wao ni wa kikazi tu kama wasanii
wengine huku wakidaiwa kuwa pamoja hasa nyakati za usiku. "Baba Haji na
Irene Uwoya ni wapenzi, wanafanya siri sana mi mwenyewe nimeshuhudia
Uwoya akimpiga mabusu ya kimahaba Baba Haji na kumuita honey,
wananunuliana mpaka zawadi, yaani mahaba yamewaelemea kabisa sema
wanashindwa tu kuweka kweupe ili dunia ijue" Chanzo hicho kiliambia
Swahiliworldplanet Juzi alhamisi.
Hata hivyo Uwoya na Baba Haji walitafutwa ili kutolea ufafanuzi madai
hayo lakini hawakuweza kupatikana mpaka habari hii inaandikwa huku
ikidaiwa Baba Haji yupo busy Zanzibar akishuti filamu mpya. Mastaa hao
wamecheza filamu kadhaa pamoja kama vile Apple na Last Card
Haji Adam 'Baba Haji"
0 comments: