|
Marehemu mchungaji DB Antrim akiwa na mmoja wa watoto wake.©Facebook/ DB Antrim. |
Huzuni kubwa imelikumba kanisa la Westwind eneo la Waukee huko IOWA
nchini Marekani baada ya kujiua kwa mchungaji mmojawapo wa kanisa hilo
ikiwa ni wiki tano kupita toka mchungaji kiongozi Brandon Barker
kumshukuru Mungu kwamba zaidi ya miaka mitano katika historia ya kanisa
hilo hawajapatwa na msiba wa muumini au kiongozi kufa.
Kwa mujibu wa daktari aliyekuwa akiuchunguza mwili wa mchungaji DB
Antrim ametangaza kutokea kutokea kwa kifo cha mchungaji huyo aliyeacha
watoto wawili wa kiume na mke mmoja bila kufafanua hasa chanzo cha kifo
chake. Kwa upande wake mchungaji Barker akizungumza kwa huzuni
|
Mke wa marehemu Allison Sherwood Antrim na mtoto wao. |
kanisani jumapili iliyopita, alisema kwamba kanisa hilo linapitia
kipindi kigumu kisichoelezeka kutokana na kifo cha mchungaji Antrim
ambaye amesema amejiua kwa mikono yake mwenyewe, na kwamba kifo hicho
hakitasahaulika katika uhai wake.
Mchungaji Barker amesema ilikuwa vigumu kukubali kwamba Antrim amefariki
siku ya alhamisi iliyopita kutokana kwamba masaa machache nyuma walikaa
pamoja kuzungumzia ujumbe atakaohubiri marehemu siku ya jumapili na
kwamba hakuwa na wazo kwamba siku hiyo ingeisha vibaya na kuwaachia
maumivu makubwa kwakuwa alishuhudia kwa macho yake mwili wa mchungaji
Antrim.
|
Watoto wa marehemu mchungaji Antrim. |
0 comments: