Star huyu wa pop atapewa tuzo hio ya heshima kwenye siku ya tuzo ambayo ni May 18 kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden Arena mjini Las Vegas.
Icon Award inatambua mchango wa msanii kwenye muziki wa pop kwenye maisha yake yote na Jennifer Lopez atakuwa msanii wa nne kupata tuzo hii na wakwanza wa kike, walio wahi kupata ni Stevie Wonder, Prince, na Neil Diamond.
J.Lo pia atapanda jukwani na kuimba wimbo wa kombe la dunia la FIFA “We Are One (Ole Ola)” na msanii mwenzake Pitbull, Wimbo mwingine atakao imba ni “First Love” kutoka kwenye album yake ya kumi A.K.A inayotoka June 17.
Watakao fanya show kwenye tuzo hizo pia ni pamoja na John Legend, Jason Derulo, 5 Seconds of Summer, Florida Georgia Line, Imagine Dragons, Luke Bryan na OneRepublic.
0 comments: