Friday, 9 May 2014

Kuhusu Uhusiano Wa Shaa Na Master J,

Mtayarishaji muziki Master J, ambaye siku ya jana kupitia Kikaangoni Live ya facebook EATV, amekiri hadharani kuhusiana na mahusiano yake na msanii Sarah Kaisi maarufu zaidi kama Shaa, ameongea na eNewz na kusema kuwa, katika siku za karibuni ataitisha mkutano na waandishi na kuweka wazi rasmi kuhusiana na kinachoendelea kati yake na Shaa na kutangaza mipango yao ya baadae.
Master J amesema kuwa, amekuwa akikutana na maswali mengi kuhusiana na yeye na Shaa na hata mama yake mzazi amemshauri kuwa, kuna haja ya yeye kuliweka suala hili wazi, na hii ikiwa ni mara ya kwanza na rasmi kabisa kwa Master J kuzungumza kuhusiana na yeye na Shaa.
j 1
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: