|
Irene Uwoya |
Habari mpya ni kuwa kuna uwezekano mkubwa mastaa wa muziki na filamu
Afrika mashariki na Afrika magharibi kukutana katika filamu mpya ya
kitanzania ambayo story yake itahusu mambo ya muziki.
Swahiliworldplanet imepenyezewa
habari hii na chanzo cha uhakika ambacho ni msanii maarufu nchini na
anayetarajiwa kuwa mmoja wa waigizaji wakuu wa filamu hiyo. Kwasasa
tayari zimeshafanyika seminar zaidi ya nne kufanya utafiti wa kutosha
kuhusu filamu hiyo ambayo kwa mujibu chanzo hicho wanataka iwe filamu ya
mwaka. Kwa mujibu wa chanzo hicho makini mpaka sasa baadhi ya mastaa
waliofikiriwa kucheza filamu hiyo ni pamoja na Professor J, Irene Uwoya,
Mariam Ismail(Tanzania), Jose Chameleon(Uganda) na muigizaji maarufu wa
Ghana Majid Michael. waigizaji wengine watatokea nchi kama kenya na
nyingine za kiafrika ambapo filamu hiyo pia inatarajiwa kushutiwa nchi
mbalimbali.
|
Mariam Ismail na Professor J |
"Wasanii wapo na mojawapo, ila bado pia majadiliano juu ya hao
wasanii yanaendelea, hapa Tanzania wasanii ambao wanafikiriwa kucheza ni
kama Irene Uwoya, Mariam Ismail, Professor J, Kutoka Uganda anafikiriwa
zaidi Jose Chameleon, Pia muigizaji maarufu wa Ghana Majid Michael
anafikiriwa sana kucheza. Na kila nchi anapotoka msanii wameona baadhi
ya vipande vishutiwe huko huko ikimaanisha itakuwa ni Ugandan, Kenya,
Ghana na Tanzania, finally vipande vingine vitashutiwa nchini
Turkey(Uturuki) ambapo kwasasa Irene Uwoya hayupo amekwenda kwenye
kazi(Uturuki) na pia kuangalia mazingira na kukubaliana na wenye
mazingira hayo itakapomalizikia filamu hiyo(nchini Uturuki), huku
wengine tukiendelea na Seminar juu ya filamu hiyo" Kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina lake.
|
Majid Michael |
0 comments: