Saturday, 10 May 2014

Jackline Wolper: Wanaosema Kifo Cha Kanumba Kimeshusha Soko La Filamu Ni Waongo.

Jackline Wolper
Muigizaji wa filamu mwenye jina kubwa nchini Jackline Wolper amesema kuwa watu wanaosema kuwa soko la filamu nchini limeshuka baada ya Kanumba kufariki ni waongo kwasababu kila mtu ana mashabiki wake na Kanumba hakuwa ameliteka soko peke yake. Wolper alisema kuwa wanaosema hivyo itakuwa ni mashabiki wa Kanumba ndiyo maana baada ya kufariki wanaona soko limeshuka kwasababu walizoea kununua kazi zake. Akizungumza katika The Sporah Show Wolper alisema .....



"Ngoja nisawazishe hapo, kila mtu ana mashabiki wake, ana msanii wake. Kuna mtu anaweza akawa anampenda Kanumba tu hampendi mtu mwingine yeyote kwa hiyo alikuwa anachukuwa movies za Kanumba tu, na kuna mwingine anaweza akawa anampenda Wolper tu ujuee!. Unajua kuna mashabiki wa hivyo ambao wanaingia hata front kupigana ukimsema Wolper, ukimsema nani? sijui nani? you know, kwahiyo mimi ninaweza nikasema huyo ni shabiki yake sana Kanumba. Kwahiyo anaona Kanumba amekufa basi ndio kila kitu kimekufa. Kama juzi hivi nimefululiza kufanya movies kama tatu na Ray, wale ambao wanasema zimeshuka labda hawajapita madukani kuangalia lakini movies zipo nyingi tu"
Wolper na Sporah
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: