Mitandao ya kijamii imewaka moto
kufuatia kanda ya video iliyozuka ikionyesha dadake mwanamuziki wa
kimataifa Beyonce Knowles , Solange Knowles akimchapa makonde
mwanamuziki Jay-Z ambaye pia ni shemeji yake katika lifti.
Wakuu wa hoteli ambako kisa hicho kinadaiwa
kutokea mjini New York, 'The Standard Hotel' wamesema kuwa wanachunguza
ambavyo kanda ya kisa kilichotokea ndani ya Lifti iliweza kusambazwa
baada ya kanda hiyo ya video kuzuka katika mtandao mmoja wa udaku TMZ.Kanda hiyo ilizuka baada ya Beyonce aliyekuwa ameambatana na Jay Z ambaye ni mumewe wa miaka sita pamoja na Solange kuhudhuria tamasha la kifahari mjini New York tarehe tano Mei.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, taarifa kutoka kwa maafisa wa hoteli ambamo kisanga hicho kilitokea walielezea kukasirishwa na mtu ambaye aliisambaza kanda hiyo kwenye internet na hata kutishia kumchukulia hatua pindi atakapojulikana.
"tumeshtushwa sana na kukasirishwa na mtu aliyekiuka sheria zetu za faragha ambazo wageni wetu wanathamini sana, '' ilisema taarifa kutoka kwa wakuu wa hoteli hiyo.
"tunachunguza hali hiyo na pia yeyote atakayepatikana na hatia ataadhibiwa vikali.''
Wasimamizi wa Beyonce walikataa kuzungumzia kisa hicho.
0 comments: