Snura Afunguka Ya Moyoni Kuhusu Diamond Kuchukua Tuzo Saba, Na Hiki Ndicho Alichosema
MSANII wa
muziki na filamu Bongo, Snura Mushi amefunguka kwamba tuzo saba za
Kilimanjaro alizopata msanii mwenzake, Nasibu Abdul alistahili kuzipata
kwani anajituma.
Akichonga na
gazeti hili, Snura alisema Diamond ni mwanamuziki anayejituma sana pia
ni mbunifu na juhudi zake ndizo zimemfanya ashinde tuzo zote hizo.
“Mimi
nilikuwa kwenye kipengele cha msanii chipukizi lakini haikuwa bahati
yangu, naamini wakati wangu ukifika nitapata tuzo sina haraka ila kwa
shemeji Diamond alistahili kupata,” alisema Snura.
0 comments: