|
Wastara akivishwa pete ya uchumba |
From London With Love ...!!! Star mkubwa wa filamu nchini
Tanzania Wastara Juma ambaye kwasasa yupo London Uingereza amevishwa
pete ya uchumba huko na mwanaume anayeonekana hapo pichani. Wastara
aliweka picha kadhaa kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii na
wengine kudhani ni filamu mpya. Star mwenzake pia Riyama Ally ambaye
wapo wote huko London nae aliandika "Ama kweli Mungu akitaka kukupa
haandiki barua......, kila la kheri mama huu mwanzo mzuri kwako". Baada
ya kuona picha hizo haraka sana
Swahiliworldplanet ilimuendea
hewani Wastara akiwa huko huko London na kumuuliza kama ni movie au ni
kweli, tofauti na siku zote ambapo kama ni movie Star huyo huweka kweupe
lakini safari hii alionekana hana la kusema pengine kwa furaha na
kuishia kujibu kwa ufupi kwa kusema "No comment" alipododoswa tena
alijibu hivyo hivyo tena "No comment".
Wastara Monalisa, Riyama Ally na Cloud ni takribani wiki tatu sasa wapo
London kwa mwaliko maalum na kucheza filamu inayoitwa Ughaibuni(Abroad)
ambapo tayari wameanza kuishuti. Tungependa kuwatakia kila la kheri
wawili hao .Angalia picha zaidi Wastara akivishwa pete
hiyo..............
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
0 comments: