Tuesday, 13 May 2014

Tazama picha, Mavazi ya 'kisharobaro' ya Mike Sonko yawavunja mbavu rais Uhuru Kenyatta na Ruto

Senator Mike Sonko ambaye amekuwa maarufu kutokana na jinsi anavyoishi maisha ya ‘kisharobaro’ aliwavunja mbavu rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na makamu wake Ruto kwa mavazi yake.

Rais Uhuru na Ruto walikuwa uwanja wa ndege wakimpokea kiongozi wa China, Li Keqiang na walipokuwa uwanjani hapo walikutana na Sonko ambaye pia alikuja kwa shughuli hiyo.

Uhuru na Ruto walishindwa kujizuia na kuangua kicheko walipomuona Sonko akiwa amevaa koti zuri la suti na tai huku chini akiwa ametupia jeans iliyochanwachawa (fashion). Rais Uhuru alionekana kwenye picha akicheka huku akinyoosha kidole kwenye jeans ya Sonko na Sonko.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: