Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO''
ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la
kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia
yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au
kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka
comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Mabaki ya kanisa la Sanjiang. ©The Telegraph |
Wakati hivi karibuni tumekufahamishwa namna gani makanisa yanafungwa na kuuzwa
nchini uingereza, huko China hali ni tofauti, kwani serikali ya nchi
hiyo imekuwa ikifanya juhudi ya kubomoa makanisa kila yanaposhamiri,
imefahamika.
Zoezi la ubomoaji likiendelea. ©International Christian Concern |
KWA TAARIFA YAKO, tukio la hivi
karibuni ni kubomolewa kwa kanisa jipya lenye uwezo wa kuchukua watu
4000 walioketi, ambapo viongozi walitoa kisingizo kwamba msalaba
uliowekwa kwenye jengo la kanisa juu kwa nje, ulikuwa mkubwa sana na
wenye kuonekana kutokea mbali kiasi cha kuwafanya watu kushindwa kutilia
maanani kile wafanyacho.
Eneo ambalo linatambulika nchini humo
kwa kuyafanya maisha ya wakristo kuwa magumu kwa njkia hiyo ni jimbo la
Zhejiang, ambapo KWA TAARIFA YAKO mnamo mwaka 2000 mamia ya makanisa na
majengo ya kuabudia wakristo yalivunjwa na uongozi wa mji huo.
Mwanzo wa tukio lenyewe inaelezwa kwamba ni pale katibu wa chama cha
Kikomunisti alipokuwa akifanya ziara kwenye mji wa Wenzhou na kisha
kuuona msalaba uliopo kwenye jengo la kanisa, ambapo aliagiza viongozi
walio chini yake kuwa uondolewe mara moja kwa kuwa ni mkubwa kupitiliza,
jambo ambalo KWA TAARIFA YAKO viongozi waliokasimishwa jukumu hilo
waliamrisha kuwa msalaba na ghorofa la kwanza la kanisa hilo libomelewe.
Ujenzi wa kanisa hilo, enzi zake. Carlos Barri/Reuters |
0 comments: