Saturday, 3 May 2014

PICHA ZA NDOA YA ANGELO BUENAVISTA WA THE PROMISE, HAKUNA FUNGATE

 

Shangwe za GK jumamosi ya leo zipo nchini Ufilipino ambako mwigizaji na mwimbaji maarufu wa nchini humo Jericho Rosales a.k.a Echo, almaarufu kwa majina ya uigizaji kama Angelo Buenavista au Christian Soriano, hatimaye siku ya alhamisi (Mei mosi) alifunga pingu za maisha na mpenzi wake wa takribani miaka miwili mwanadada Kim Jones mwenye asili ya Uingereza na Ufilipino ambaye kifani ni mwanamitindo nchini humo.
Ndoa hiyo iliyosubiriwa kwa hamu na watu waliowengi hasa kipindi hiki ambacho Jericho jina lake linavuma kwa mara nyingine kutokana na tamthilia mpya inayoendelea kuonyeshwa nchini humo iitwayo The Legal Wife, imefungwa katika ufukwe wa Boracay nchini Ufilipino na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wa wana ndoa hao. Lakini pia siku moja kabla ya ndoa hiyo mpenzi wake wa zamani ambaye kwasasa ni mke wa mtu mwanadada Kristine Hermosa almaarufu kama Yna Macaspac au Arrabella alimtumia salamu za kumtakia heri Jericho katika siku yake hiyo kubwa, kwasasa mwanadada huyo yeye ni mjamzito wa miezi mitatu na kwa mujibu wa vipimo alivyochukua wiki hii yeye na mumewe wanatarajia kupata mtoto wa kiume, ambaye atafanya jumla awe na watoto watatu, wawili wa kuzaa na mmoja alimuasili kutoka kituo cha watoto yatima.
Pamoja na harusi hiyo kufungwa mwigizaji huyo hakuwa na jinsi zaidi ya kusogeza mbele fungate(honeymoon) yake kutokana na kuhitajika kwenda kurekodi vipande vingine vya tamthilia hiyo kutokana na kazi yake kutokamilika kulikotokana na tufani iliyotokea nchini humo miezi ya karibuni. Kitendo hicho cha kusogeza mbele fungate pia kimeombwa radhi na mwigizaji mwingine nyota katika tamthilia hiyo Angel Locsin. Kabla ya harusi hii Angelo amewahi kuwa na uhusiano na wasichana tofauti na kujikuta akipata mtoto katika umri wa miaka 21, ambapo ameungama dhambi zake na kwasasa maisha yake ameyatoa kwa Mungu, na kutaka kuishi maisha yanayompendaza aliyejuu.
Ukitaka kusoma na kuona walivyovalishana pete ya uchumba kanisani BONYEZA HAPA. Tazama picha mbalimbali za harusi ya Jericho Rosales na Kim Jones (echokimforever)


Jericho akijaribu vyombo vitakavyotumiwa na bendi katika harusi yake.
Madhabahu ikiwa imepambwa tayari kwa ndoa.
Kim akiwa tayari kuelekea sehemu ya tukio.
Ua maalumu likiwa katika suti ya Jericho.
Wadada wasimamizi wakiwa katika pozi.
Wapambe na marafiki wakipata picha ya pamoja na Jericho.

Bwana harusi Jericho akiingia tayari kwa ndoa.
Picha zikimuonyesha Jericho akiingia sehemu maalumu kwaajili ya ndoa yake.
Jericho akiwa mwenye furaha.
Kim akiwa anaingia akisindikizwa na kaka yake.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: