MWANAMUZIKI mwenye sauti ya mvuto, Ray C, amelazwa katika
hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam akikabiliwa na homa kali.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, mwanamuziki huyo
ambaye amekuwa katika tiba ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya
hospitalini hapo, alifikishwa hapo jana Jumatatu asubuhi na baadhi ya
madaktari walibainisha kuwa Ray C anasumbuliwa na ugonjwa wa dengue
ambao umelipuka katika maeneo mengi jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
“Tumemfanyia vipimo, ana homa kali sana lakini
hana malaria. Baada ya kuchunguza dalili, tumechukua vipimo na kubaini
kwamba amepata maambukizi ya dengue, hivyo tunaendelea kumpa matibabu
kwa sasa,” alieleza daktari ambaye hakutaka kutajwa jina lake.
Mwanaspoti iliyofika wodini alimolazwa mwanamuziki
huyo, lilijaribu kuzungumza naye, lakini manesi wazuia wa kusema
hapaswi kuamshwa kwa kuwa alikuwa amepewa dawa za kutuliza maumivu na
kushusha homa.
Ray C amekuwa katika tiba ya kuacha dawa za
kulevya na amekuwa akisaidiwa kurejea katika sanaa ya muziki ambayo
alikuwa akiifanya vizuri kabla ya kuingia kwenye wimbi hilo.
Ugonjwa huo dengue uliotajwa kumsumbua kwa sasa
umewakumba wananchi wengi wa Dar es Salaam na unaenezwa na mbu weusi
waitwao Aedes Egypitia.
Mbu hao ambao huonekana zaidi mchana, huzaliana katika maji safi yaliyotuama.
Usiku wa kuamkia juzi Jumapili, Ray C alikuwapo
kwenye ukumbi Mlimani City kwenye hafla ya Tuzo za Muziki za Kilimanjaro
ambapo hakuonekana kuwa na dalili zozote za kuumwa.
Credit:Mwanaspoti
Credit:Mwanaspoti
0 comments: