Monday, 5 May 2014

MKALI WA KWA NEEMA I EDSON ZAKO MWASABWITE ANUSURIKA KWENYE AJALI YA GARI


Weekend hii pamoja na kusheherekea tamasha la pasaka katika mkoa wa Shinyanga, Edson Zako Mwasabwite anamshukuru Mungu kwani ni makubwa yangekuwa yamempata hadi hivi sasa. 
Muimbaji huyu nyota anayejulikana kwa wimbo wa "Ni kwa Neema tu" akitokea Dodoma kwenda Morogoro siku ya Jumamosi tarehe 3 Mei, ndipo ajali ilitokea na maeneo ya Gairo, mwendesha bodaboda akiwa amembeba abiria walikatiza barabarani, ndipo hapo katika jitihada za kumkwepa akawa amemgonga, (abiria akaishia kwenye kioo cha gari, airbag zikafunguka hata asiweze kuona mbele hadi alipogota kwa kugonga gogo) ambapo mwenye bodaboda na abiria wake waliumia kiasi cha kupelekwa hospitalini (na kugundulika na polisi ya kwamba walikuwa wamelewa), ambapo wapo hadi hivi sasa, huku gari yake ikiwa kituo cha Polisi Gairo.
Edson akizungumza na GK, ameeleza kuwa anamshukuru Mungu maana ni mwema, hakika ni kwa Neema tu bado anaishi, ambapo alitoka salama, akiwa na maumivu ya shingo tu hadi hivi sasa, ambayo yanaendelea kutoweka
Edson Mwasabwite na Faraja Ntaboba kwenye tamasha la pasaka jijini Mwanza.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: