Tangu wasichana 276 wa Nigeria walipotekwa nyara na kundi la Boko Haram, watu mbalimbali maarufu duniani wamepost picha kwenye mitandao ya kijamii wakiwa na mabango yaliyoandikwa ‘Bring back Our Girls’, ikimaanisha wanajiunga na kampeni ya raia wa Nigeria.
Mwana mitindo Irina Shayk ambaye ni mpenzi wa mchezaji wa mpira wa
miguu Christian Ronaldo yeye amepost picha kwenye twitter na Instagram
akiwa amepoz mtupu huku akiwa ameshikilia bango linaloonesha amejiunga
na kampeni hiyo, na bango hilo ndilo lililofunika kifua chake.
Hata hivyo kitendo chake hakikuungwa mkono na baadhi ya followers
wake ambao walionesha moja kwa moja hisia kwa kumshambulia kuwa ameenda
kinyume na maadili.
“Pretty tasteless and disrespectful. No class. This is exactly the justification terrorists are probably using to prevent women from receiving 'western education.” Aliandika mtu mmoja.
Mwingine aliona kama amefanya dharau kwa kuwa tatizo hilo sio la nchi
kubwa kama Marekani na kuhoji kama angediriki kufanya hivyo siku ya
tukio kubwa la shambulizi la kigaidi la September 11 nchini Marekani.
“Would you stand there n*ked wishing sorrow on the 9/11 victims?
Would you do it for the tsunami? This is a tasteless attitude to 200
missing girls.”
Hata hivyo sio wote waliomshambulia, wengine walimsapoti na kueleza
kuwa alikuwa na nia njema ya kuvuta umakini zaidi wa watu kuifuatilia
kampeni hiyo kwenye mitandao ya kijamii.
0 comments: