Thursday, 8 May 2014

Muigizaji anayekula udongo kila siku


Udongo
Muigizaji mashuhuri wa Hollywood nchini Marekani, Shailene Woodley, mapema wiki hii aliwashangaza watu alipofichua kuwa yeye hula udongo kila siku kwa kupima kijiko kimoja.
Lakini je ni sawa kula udongo kwa sababu za kiafya?
Muigizaji huyo, aliyewahi kucheza filamu mashuhuri ya Descendants akishirikiana na George Clooney, alisema kuwa udongo ni moja ya vitu vyenye afya kwa mwili ambavyo yeye mwenyewe anaweza kula.
"nimegundua kuwa udongo unaweza kukupa afya nzuri mwilini. Najua wengi wanadhani kuwa mimi ni kichaa ninaposema kwmaba , udongo una uwezo wa kusaidia kusafisha mwili wako kutokana na madini mazito mwilini,'' alisema Woodley.
Anasema alijifunza kula udongo kutoka kwa dereva mmoja mwafrika. Baadhi ya marafiki zake hutengeza dawa ya kusugua meno kutoka kwa udongo ambao unaweza kumeza. Hata hivyo alisema ni muhimu kuwa udongo huo kabla ya kuliwa uwe safi.
Tabia ya kula mchanga au udongo inajulikana kwa kiingereza kama Geophagy.
Shailene Woodley
Ni jambo la kawaida watu kula udongo Afrika au Mashariki ya kati ingawa sharti uwe yametengezwa kwa mfano wa tembe. Hii ni kwa mujibu wa mtaalamu wa afya katika hospitali ya Kings College, London, Rick Wilson.
Sababu muhimu ambayo inaweza kukufanya kula udongo ni kukosa madini ya ZINC mwilini, lakini wataalamu wanasema kukosa madini hayo mwilini sio hatari na kwamba sio jambo la kawaida barani Afrika watu kukosa sana madini hayo mwilini.
Lakini Shailene Woodley anaamini kuwa kula udongo inaweza kukupa afya nzuri.
Udongo hata unaweza kuathiri mwili wako hasa ikiwa una chembechembe za Arsenic au Lead.
Wanawake wajawazito wakati mwingine hupata hamu ya kula udongo au mkaa kwa kukosa madini fulani mwilini,anasema daktari Sartah Jarvis.
Na inaweza kueleweka ikiwa ni barani Afrika kwa sababu ya changamoto ya lishe bora lakini kula tu udongo kwa sababu ya kupenda , hiyo haiwezekani.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: