Ndege ya kijasusi ya Uingereza
iliyokuwa katika harakati za kutafuta zaidi ya wasichana miambili
waliotekwa nyara nchini Nigeria, imelazimika kutua nchini Senegal
kutokana na hitilafu.
Ndege hiyo iliondoka Uingereza Jumapili kujiunga
na juhudi za kimataifa za kuwatafuta wasichana waliotekwa nyara na Boko
Haram na sasa imetua nchini Senegal kutengezwa.Wasichana hao walitekwa nyara zaidi ya wiki tano zilizopita na kundi la wapiganaji waisilamu la Boko Haram.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Marekani na Israel zinasaidia jeshi la Nigeria kwa ujasusi katika harakati za kuwasaka wasichana hao ambao Boko Haram inataka serikali ya Nigeria ibadilishane na wafungwa wa kundi hilo.
Jeshi la Marekani linatumia ndege zenye rubani na zile zisizo na rubani kusaidia juhudi za Nigeria kuwatafuta wasichana hao
0 comments: