Polisi nchini Nigeria wameahidi
kumtunuku dola laki tatu za marekani yeyote atakayetoa habari
zitakazowasaidia kuwapata zaidi ya wasichana mia mbili waliotekwa na
kundi la wapiganaji wa boko haram mwezi uliopita .
Juma lililopita Wapiganaji wa Boko Haram
walisema kuwa wasichana hao 200 kutoka eneo la Chibok waliotekwa mwezi
uliopita watauzwa.8 kati yao walitekwa kutoka kijiji cha Warabe kilichoko katika jimbo la Borno siku ya jumapili nao watatu zaidi wakatekwa kutoka kijiji jirani .
Rais wa Marekani ameingilia swala hilo akisema kuwa serikali yake itatoa msaada ili kuwakomesha wapiganaji hao.
Tayari marekani imewatuma maafisa kadhaa kusaidia kusuluhisha kwa amani kitendawili cha utekaji nyara huo.
Wakati haya yakijiri, taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa mamia ya watu waliuawa katika shambulizi lililofanywa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon siku ya Jumanne.
Katika mahojiano na BBC kiongozi mmoja wa eneo hilo, Ahmed Zanna, alisema kuwa washukiwa walivamia mji wa Gamboru Ngala, katika jimbo la Borno, na kuwaua takriban watu 300.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa wamepata zaidi ya maiti miamoja kutokana na shambulizi hilo.
0 comments: