Siku ya jana nimekutana na mkosi wa aina yake ilikuwa mida ya saa 7 mchana nikitoka Sinza kuelekea Posta kufanya yangu . Ndipo
daladala ilipofika maeneo ya Magomeni alipanda jamaa mmoja kiukweli
daladala haikuwa na abiria wengi kwani kulikuwa na siti za wazi nyingi
na mimi nilikaa mwisho kabisa wa daladala cha ajabu na kilichonishangaza
jamaa kaacha siti zote kaja kukaa na mimi akasema samahani kaka siti za
mbele huwa sizipendi huku anachekacheka.
Akaanza kuniuliza kila kituo tukifika eti hapa ndo wapi,Maria leo fire
foleni hamna,mara nimechelewa kazini nikifika tu navaa unform haraka
alivyoona niko kimya akasema kaka vipi mbona we mpole hivyo
nikajichekesha kidogo nikamwambia kawaida tumefika Jangwani akaanza
kunitongoza kaka unaitwa nani,unaishi wapi,we ni last born nini umepanga
au unaishi kwa wazazi alafu umependeza,nataka uwe mume wangu pesa
ninazo.
Kiukweli uzalendo ulinishinda nilijikuta
ninemfokea kwa nguvu na kumtusi matusi ya maana sijui hata yalipotoka
hayo matusi aibu ilimjaa sana jamaa ikawa habari ndani ya daladala.
Ilinibidi nishuke kituo ambacho sikupashwa kushuka,watu wengine mikosi sana.
0 comments: