Wednesday, 7 May 2014

Shughuli ya kupiga kura yaanza Afrika Kusini


Chama tawala ANC kinatabiriwa kushinda uchguzi huu licha ya kashfa nyingi tu
Shughuli ya kupiga Nchini Afrika Kusini ilianza vyema mapema leo asubuhi huku idadi kubwa ya wapigaji kura ikijitokeza.
Zaidi ya watu million 25 nchini humo wanaendelea katika vituo vya upigaji kura kwa uchaguzi mkuu wa mara ya tano tangu kumalizika kwa utawala wa mtu mweupe.
Chama tawala cha African National Congress, ANC ndicho kilicho maarufu zaidi. Lakini umaarufu wa chama hicho na rais Jacob Zuma umeathirika kutokana na tuhuma za rushwa na matatizo ya kijamii.
Licha ya kukumbwa na kashfa za ufisadi na utawala mbovu, duru zinasema kuwa chama cha ANC huenda kikanyakuwa ushindi.
Uchaguzi huo unasimamiwa na maafisa zaidi ya 200,000 wa tume ya uchaguzi watakao zunguka mikoa yote 9 iliyoko nchini.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema kuwa raia wengi wa Afrika Kusini bado wanakipenda chama cha ANC,kwa sababu kimeweza kuweka udhibiti na kujali masilahi ya wananchi masikini.
Anasema kuwa kifo cha Nelson Mandela huenda kimeipa ushaiwishi mkubwa chama hicho.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: