Kipa wa Tanzanite akiwa ameshikwa wakati akitaka kukimbia baada ya kumshushia kipigo Refa
MBOZI,
MBEYA
Jana wa vwawa uliopo Wilaya ya mbozi jijini mbeya kunaendelea mashindano
ya ligi daraja la pili katika ngazi ya mabingwa wa mkoa. Ligi hiyo
ikiwa imefikia katika mzungukowa tano hivi leo ambao umewakutanisha Timu
mbili kutoka kanda ya Kaskazini ambazo ni AFC kutoka jijini Arusha na
timu ya Tanzanite Fc kutoka mkoani Manyara.
Katika mchezo huo ulioanza kwa kasi mnamo saa nane kamili, Ukiongozwa na
muamuzi ndugu Bitebo Manduta huku kila timu ikionesha hari ya kuibuka
na ushindi ndipo hali ilipobadilika mnamo dakika ya 15 pale AFC
ilipoandika Goli lake la kwanza.Mpaka dakika ya 38 kipindi chakwanza AFC
ilipoongeza Goli lapili mpakakipindi chakwanza kilipokwisha matokeo
bila kubadilika.
Katika Kipindi cha pili kilipoanza Timu ya Tanzanite ilionesha
mashambulizi huku kukiwa na uwalakini kila walipofika katika lango la
Timu pinzaniwalionekana kusuasua kufunga kitendo kilichohamsha hisia
tofauti kwa mashabiki huku wakipiga kelele kuwa wameuza mechi. Kelele
hizo zilizua taharuki nakusababisha mashambulizi yaliyozua makosa ya
mchezaji wa Tanzanite ndipo refa alipompa adhabu ya kadi ya njano
kitendo ambacho kilisababisha Wachezaji wa Tanzanite kumzonga refa huku
wakitoa maneno ya kejeli. Jitihada ya Refa kuwatuliza ziligonga mwamba
ndipo alipoongezaadhabu kwa mchezaji na kumpa kadinyekundu kitendo
kilichoashiria kuwa walikua wakisubiria kadi hiyo ndipo walipoanza
kumshushia kipigo Refa huyo. Na kuokolewa na Polisi wa kutuliza ghasia
aliokua uwanjani hapo na kufanikiwa kuwakamata wachezaji watatu
waliomshambulia Refa huyo.
Hata hivyo nilipata fursa ya kuzungumza na muamuzi aliyekua akitazama
mpira katika benchi la mashabiki juu ya hatima ya timu ya Tanzanite na
wachezaji waliotiwa nguvuni aliweza kubainisha kuwa kutokana na kanuni
za michezo kwakosa hilo kuna uwezekano wa timu husika kunyang'anywa
pointi zao na kufungiwa kabisa ila pia aligusia kidogo kuhusu wachezaji
waliotiwa nguvuni kuhusika na shambulio hilo dhidi ya muamuzi alisema
kwa kuwa muamuzi kaelekea polisi sasa hiyo ni kesi na ni kesi ya jinai
ya kushambulia na kudhuru mwili hadharani na kesho weachezaji hao wana
uwezekano wa kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka hayo.story na https://www.facebook.com/cassim.mwinyi?fref=ufi | | | | | | | | | | | | |
|
0 comments: