Lil Wayne, Birdman na washkaji wote wa Young Money Entertainment wamesema hawatamtenga Justin Bieber licha ya kuenea kwa video zake za ubaguzi wa rangi.
Rais wa Young Money, Mack Maine ameuambia mtandao wa TMZ kuwa kila mmoja kwenye label amewahi kuwa karibu na staa huyo na hajawahi kuonesha dalili zote za kibaguzi. Mack Maine amesema marafiki wengi wa Justin ni weusi na kwamba huishi na kila mtu kwa usawa.
Ameongeza kuwa Justin amekuwa akiendana na tamaduni za hip hop na za watu weusi na kuongeza kuwa kila mmoja kwenye kambi ya Young Money anaamini kuwa umri wa Bieber kipindi anatoa kauli hizo hauendani.
Kwa sababu hizo Mack amesema Young Money itaendelea kufanya kazi naye.
0 comments: