WATU
wawili wamefariki dunia mkoani Kilimanjaro katika matukio tofauti,
likiwemo la mmoja aliyekutwa amekufa akiwa katika basi la Kampuni ya
Kilenga akiwa safarini kuelekea mkoani Arusha.Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Moita Koka, alisema kuwa mtu huyo
ametambuliwa kwa jina la Sayuni Joel (53), mfanyabiashara, mkazi wa
Mwembe, wilayani Same, Kilimanjaro.
Akizungumzia
mazingira ya tukio hilo, Kamanda Koka alisema Joel alipanda basi hilo T
398 BAT na kwamba kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa akisumbuliwa na
tumbo na alikuwa akielekea hospitali kupata matibabu.
Alisema Joel aligundulika kuwa amepoteza maisha baada ya gari hilo kuingia katika stendi kuu ya mabasi Moshi.
Maiti yake imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC huku uchunguzi wa chanzo cha kifo hicho ukiendelea.
Katika
tukio jingine, mkazi wa Kijiji cha Kilema – Kiyou, Kata ya Kilema,
wilayani Moshi, Martin Michael (45), amekufa baada ya kujinyonga kwa
kutumia kamba ya chandarua.
Mashuhuda
wa tukio hilo walisema lilitokea juzi, saa 8 mchana na kudai kwamba
amefikia uamuzi huo kutokana na kuchoshwa na hali yake kiafya ambayo
imemfanya kutumia dawa kila mara na kwamba kabla ya tukio hilo aliwahi
kusikika akilalamikia hali hiyo.
Na Dixon Busagaga, moshi
0 comments: