Mwanamke
mmoja wa Tennessee, Marekani hivi karibuni aliamua kufanyakitendo
ambacho huenda kwake aliamini kuwa ni ubunifu utakao wa ‘wow’ wageni
waliohudhuria kanisani kushuhudia ndoa yake na mume wake ikifungwa.
Mwanamke huyo aitwaye Shona Carter-Brooks aliingia kanisani na mwanaye
mwenye umri wa mwezi mmoja, lakini sio kwa kumpakata mikononi kama
ilivyotarajiwa na wengi, bali alimuweka kwenye mkia wa shela yake na
kumburuta katika sakafu ya kanisa wakati yeye na mume wake walipokuwa
wakiingia kanisani kuelekea kwenye ‘altar’.
0 comments: