ZIKIWA zimekatika siku 40 tangu kifo cha muongozaji maarufu Bongo, George Otieno ‘Tyson’, mke wa ndoa wa marehemu, Yvonne Sheryl ‘Monalisa’, mama yake mzazi , Suzan Lewis ‘Natasha’ pamoja na mwanaye Sonia wamefanyiwa sherehe.
Mke wa ndoa wa marehemu Tyson, Yvonne Sheryl ‘Monalisa’ akiwa katika picha ya pamoja na mwanaye Sonia.
Mke wa ndoa wa marehemu Tyson, Yvonne Sheryl ‘Monalisa’ akiwa katika picha ya pamoja na mwanaye Sonia.
Kwa mujibu wa Monalisa, sherehe hiyo ni ya kimila kwa upande wa kabila lao la Kizaramo ambapo wenyewe huita shughuli ya kuoshwa.Shughuli hiyo iliyokusanya mastaa kibao ikiongozwa na Team Monalisa na Team Natasha ilifanyika wikiendi iliyopita nyumbani kwa Monalisa, Yombo – Buza jijini Dar es Salaam.
Katika shughuli hiyo ambayo ilihudhuriwa na mwandishi wa habari hizi, wafiwa hao waliingizwa bafuni na kuogeshwa kisha kuvalishwa nguo mpya na kutolewa nje, zoezi ambalo lilifanyika chini ya usimamizi wa mkongwe wa maigizo nchini, Zawadi.

…zawadi zilianza kutolewa kwa wakina Monalisa.
Muongozaji wa shughuli hiyo, Mama Abdul alisema nia ya kuwaosha wafiwa hao ni mila na desturi ya Kabila la Kizaramo na kwamba wao kama marafiki wa karibu waliamua kuwafanyia wenzao kwa lengo la kuwapa moyo baada ya kuwa kwenye matatizo.
…wakina Monalisa haoo… wakiendelea kutunzwa na kupokea zawadi mbalimbali.
…wakina Monalisa haoo… wakiendelea kutunzwa na kupokea zawadi mbalimbali.
“Nguo na fedha tulizotoa hapa ni kuonyesha kuwa tunajua kuwa walikuwa kwenye matatizo na sasa tunawapa nguvu ili waanze maisha yao mapya bila ya mpendwa wao. Tunajua ni ngumu sana kibinadamu, ndiyo maana tumesisitiza kuwa, dua ni muhimu kwa wenzetu,” alisema mama Abdul.
…kama kawaida wakati wa maakuli mambo yalikuwa hivi.
…kama kawaida wakati wa maakuli mambo yalikuwa hivi.
VILIO UPYA
Katika shughuli hiyo, Monalisa alishindwa kujizuia na kujikuta akiangua kilio, hali iliyosababisha hata mwanaye Sonia aungane naye, lakini mashosti zake walimtuliza.
Katika shughuli hiyo, Monalisa alishindwa kujizuia na kujikuta akiangua kilio, hali iliyosababisha hata mwanaye Sonia aungane naye, lakini mashosti zake walimtuliza.
NATASHA ATOA NENO
Mama wa Monalisa, Natasha alisema: “Namshukuru sana Mungu kwa uwezo wake, kutujalia nguvu katika kipindi hiki kigumu kwa familia yetu, hasa mwanangu Monalisa na mwanaye Sonia.
Mama wa Monalisa, Natasha alisema: “Namshukuru sana Mungu kwa uwezo wake, kutujalia nguvu katika kipindi hiki kigumu kwa familia yetu, hasa mwanangu Monalisa na mwanaye Sonia.
“Pia tumefarijika sana na ujio wenu marafiki zetu. Tunajua mlikuwa na mambo mengi ya kufanya lakini mmeona kuna umuhimu wa kuungana nasi na kutupa moyo. Mwenyezi Mungu awazidishie. Huu ndiyo urafiki wa kweli.”
0 comments: