Mwimbaji mahiri wa muziki wa Injili, Ephraim Sekeleti, atatumbuiza kwenye uzinduzi wa alamu ya ‘Kamata Pindo la Yesu’ ya Rose Muhando Agosti 3, mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Taarifa kwa vyombo vya habari aliyotoa Rose Muhando jana, ameeleza kuwa tayari Kampuni ya Msama Promotions inayodhamini uzinduzi wake imeshamalizana na mwimbaji huyo.
“Nashukuru sana Msama Promotions kwa udhamini wao, na jana (juzi) wamenihakikishia wameshamalizana na Sekeleti na amekubali kuja kuungana nami katika uzinduzi wangu. “Ni msanii mwenye uwezo mkubwa, ambaye mashabiki wangu watapenda kuja kumuona jukwaani,” alisema mwimbaji huyo na kuzitaja baadhi ya nyimbo maarufu za Sekeleti kuwa ni Uniongoze na Kidonge cha Yesu.
0 comments: