MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Winfrida Josephat maarufu kama Rachel, amekanusha uvumi kuwa anatoka kimapenzi na mkongwe wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Winfrida Josephat maarufu kama Rachel,
Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), aliyetamba na kibao chake cha Kizunguzungu, alisema maneno hayo siyo mageni kwake, lakini ukweli ni kwamba hawana uhusiano wa kimapenzi, isipokuwa amemuweka katika mipango ya kuja kufanya kazi na mkali huyo wa singo iliyotamba sana ya Zeze.
Mkongwe wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’.
Aidha alisema katika maisha yake ya kila siku, hategemei kuhongwa vitu au hela na wanaume, ila baada ya kupata mafanikio kupitia sanaa, anaitumia kama mtaji wa kufanya shughuli nyingine za kumuingizia kipato na hivyo kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yake.
0 comments: