Wednesday, 16 July 2014

MAPYA YAIBUKA!! RICH MAVOKO AUKANA WIMBO WAKE MPYA ULIOTOKA HIVI KARIBUNI, SOMA HAPA


 


Rich Mavoko amekana kuachia wimbo mpya unaoitwa ‘Tururu’ wimbo ambao ulisambaa sana jana kwenye mitandao ya kijamii na websites na kupata namba nzuri ya watu walioupakuwa. Akiongea na tovuti ya Times Fm, Rich Mavoko amesema binafsi ameshangaa baaad aya kusikia kuwa ametoa wimbo mpya na kwamba wimbo huo sio wimbo mpya, ni wimbo aliourekodi miaka mitano iliyopita na hana mpango wa kuutoa. “Sio ngoma mpya, cha kwanza nachoweza kusema. Si ngoma ambayo nimeitoa mimi. Yaani sijui nani ameileta, blog gani inafanya hivyo vitu. Kwa sababu ni ngoma ambayo nimeirekodi miaka mitano nyuma. Can you imagine ni ngoma ambayo nimeifanya hata kabla sijafanya Silali.” Rich Mavoko ameiambia tovuti ya Times Fm. Ameeeleza kuwa hii sio mara ya kwanza watu kuvujisha nyimbo zake na yeye anaonekana kama anavujisha ngoma.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: