Ndani ya hifadhi ya Eland Game Reserve iliyoko KwaZulu-Natal,
South Africa mwendesha baskeli alikatisha siku ya June 14 2015,
akakutana na chatu mkubwa mzima kabisa aliyeonekana kama amekula na
kushiba kupita kiasi… akampiga picha na kushare na watu wake mitandaoni.
Watu wengi walisogea pia nao kujionea tu
jinsi chatu huyo alivyo kwa sababu sio kawaida unaweza kukutana na
Chatu alafu akakuacha hivihivi… Siku sita baadae yule chatu alikutwa
amekufa, wakaja walinzi wa hifadhi hiyo wakampasua ili kujua nini
kilichomfanya afe !!
Kumbe chatu alikula nungunungu.. ndani
ya tumbo kakutwa nungunungu huyo japo hawana uhakika kama ni kweli
nungunungu kasababisha kifo cha chatu huyo.
0 comments: