Leo headlines zimerudi tena huko Nigeria baada ya watu 10 kuwekwa karantini katika hospitali ya Calabar huku mtu mmoja akifariki baada ya kuwa na dalili zote za ugonjwa huo.
Vyombo vya habari vya Nigeria vimesema mtu huyo alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali.
Hivi karibuni Shirika la afya duniani WHO lilitoa taarifa kuwa nchi tatu zilizokuwa zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo ambazo ni Guinea, Sierra Leone na Liberia mpaka sasa zimefanikiwa kukaa bila kuwa na tukio lolote la ugonjwa wa Ebola.
Ugonjwa huo ulianza kushika kasi Machi mwaka 2014 na zaidi ya watu 10,000 wamefariki dunia kwa ugonjwa huo.
0 comments: