Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi
wa Msumbiji wakigonga glasi ya kutakiana heri wakati wa dhifa ya
kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake katika
ikulu ya nchi hiyo jijini Maputo maarufu kama Ponta Vermelha usiku wa
kuamkia leo.Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaaga wananchi wa
Msumbiji akisisitiza kuwa uhusiano wa kidugu na kipekee kati ya nchi
hizo mbili utaendelea kudumu na kukua
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi
wakisimama wakati nyimbo za Taifa zikipigwa wakati wa dhifa ya kitaifa
iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake katika ikulu ya
nchi hiyo maarufu kama Ponta Vermelha usiku wa kuamkia leo.Mstahiki Meya wa Jiji la Maputo Mh.David Simango akimvisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete vazi maalum na kumkabidhi Ufunguo wa jiji la Maputo kama ishara ya kumtunuku ukazi wa kudumu wa heshima wa jiji hilo wakati wa hafla iliyofanyika katika Jumba la Halmashauri ya jiji la Maputo
Mstahiki Meya wa Jiji la Maputo Mh.David Simango akijiandaa kumpa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ufunguo wa jiji la Maputo kama ishara ya kumtunuku ukazi wa kudumu wa heshima wa jiji hilo wakati wa hafla iliyofanyika katika Jumba la Halmashauri ya jiji la Maputo.
0 comments: