kulia ni dogo janja akiwa na madee |
Msanii Madee kuachia dude jipya lililopewa jina la ‘Mguu Pande’ baada ya kuhakikisha Dogo Janja amesimama
Ni baada ya kumaliza kazi ya kumrudisha
Dojo Janja katika game , msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection,
Madee Ali, anarajia kuachia wimbo wake mpya uitwao Mguu Pande.
Akizungumza na moja ya mtandao Jumanne
hii, Madee amesema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kumrudisha Dogo Janja,
hivyo kinachofuata kutoka Tip Top ni ujio mpya wa Madee.
“Kwanza tunawashukuru watanzania pamoja na media zote kwa kupokea vizuri kazi mpya ya Dogo Janja,” alisema Madee.
Aliongeza, “Sasa baada ya Dogo Janja, mimi nakuja hivi karibuni.
Kuna wimbo unaitwa Mguu Pande nimefanya na Tuddy Thomas na kazi ipo tayari kutoka.”
Video ya wimbo mpya wa Dogo Janja ‘My Life’ unafanya vizuri baada hivi karibuni kutrend nchini Nigeria.
0 comments: