Friday, 18 March 2016

Serikali yafafanua ushindi wa tuzo ya muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu'

post-feature-image

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imefafanua kwamba filamu ya ‘Mapenzi ya Mungu’ ya msanii Elizabeth Michael (Lulu) iliyoshinda tuzo ya Filamu bora Afrika Mashariki mapema mwezi huu huko Lagos, Nigeria katika tuzo za African Magic Views Choice Award (AMVCA), aliipata kwa kuwa yeye ndiye mmiliki wa filamu hiyo.

Taarifa kutoka wizara hiyo zimeeleza kwamba, filamu hiyo imetengenezwa chini ya Kampuni ya Proin Promotion na imesajiliwa kwa namba ya usajili CO831190 na Lulu ndiye mwenye haki zote za umiliki wa filamu hiyo ndiyo maana alipata tuzo hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba, ili filamu ikamilike inahusisha watu mbalimbali wanaoshirikishwa kukamilisha filamu kuanzia mtoa wazo, muswada na mtaalamu jambo ambalo haliondoshi umiliki wa
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: