Mgombea
wa urais kupitia chama cha CCM Visiwani Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein
ameshinda kiti cha urais kwa jumla ya kura 299,982 awa na asilimia 91.4
ya kura zote halali 328,327 katika uchaguzi wa marudio uliofanyika jana.
Matokeo hayo yametangazwa leo na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha.
Uchaguzi
huo wa marudio ulifanywa jana baada ya kufutwa Oktoba 25 kutokana na
kile kilichotangazwa na Jecha kuwa ni kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa
taratibu za uchaguzi huo.
Uchaguzi huo ulisusiwa na vyama kumi kwa kile walichodai kuwa kufutwa kwa uchaguzi huo mwezi Oktoba ilikuwa ni batili.
Hata hivyo karatasi za kupigia kura zilikuwa na majina yote ya wagombea kama ilivyokuwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba.
Jecha alifafanua kuwa hakuna hata mgombea mmoja aliyefuata utaratibu wa kujitoa kwa mujibu wa sheria na kanuni.
==> Matokeo yote kama yalivyotangazwa yako hapo chini....
Endelea Kutembelea Mpekuzi kwa habari motomoto..!
0 comments: